DOWNLOAD  $0.99

Fiqhi ya Ibada - Hija

  Fiqhi ya Ibada - Hija icon

  Fiqhi ya Ibada - Hija

  by: 0 0

  DOWNLOAD  $0.99

  Screenshots

  Description

  Ibada ya Hijja kwa njia ya picha: ni sehemu katika mradi wa ‘Fiqhi Ibada yenye picha’

  Lengo la ‘Tatbiiq’ ni kumuwezesha mwanafunzi kufahamu namna ya Hijja ya Mtume ilivyokuwa kuanzia anapohirimia hadi anapomaliza Hijja yenyewe na kurudi kwake. Kila tukio na ibada katika Hijja kinaangaliwa kama vile Mtume yupo miongoni mwetu akiitekeleza; ‘Tatbiiq’ inaanza na Hajj kufika Makka na nafasi yake na fadhila zake, kisha inaingia katika Hijja yenyewe na kuangalia kipengele kimoja hadi kingine kwa utulivu; maana ya Hijja, ‘Umrah hukumu na fadhila zake, kisha Miiqat kwa aina zake sehemu na wakati na kila kinachohusiana nacho. Baada ya hapo mwanafunzi atajifunza kuhirimia; maana yake, kinachoruhusiwa na kukatazwa baada yake, kisha Nask, talibiya na yanayohusiana nayo. Baada ya hapo atasoma nguzo za Hijja, wajibu na sunna zake, na kadhalika ‘umrah, nguzo zake, wajibu wake na sunna zake, hadi atakapofikia kwenye fidiya na Hadyi, kisha udh-hiya; maana yake, hukumu zake wakati wa kuchinjwa kwake na vigawanyo vyake. Mwishowe ziara ya Hujaji Madina na kabla ya kurudi kwake, na yanayohusiana na ziara na hukumu zake, taratibu zake makosa yanayoweza kutokea na hadhari zote zinazohusiana na ziara ya Hujaji Madina.

  www.fiqhiswahili.com

  Nakala iliyotimia ya ‘Tatbiiq’ ya fiqhi Ibadat yenye picha inakusanya yafuatayo:

  1-Zaidi ya video 55 za mafundisho
  2-Kiasi cha masomo 57
  3-Mamia ya picha yenye maelezo na mafundisho

  Fiqhi hii ya utekelezaji inasifika kwa yafuatayo:

  1-Uwezekano wa kutafuta Nasw yoyote, pamoja na uwezo wa kutafura aya na Hadithi mbali mbali.
  2-Chaguzi mbali mbali za vyombo vya uratibu
  3-Uwezo wa kuweka mwanga wakati wa kusoma
  4-Viweko ambayo unaweza kuweka masomo yaliyokupendezesha na video mbali mbali kwa urahisi wa kuyarejea.
  5-Urahisi wa utumaji wa uyapendayo kwa marafiki zako kwa njia ya barua pepe.
  6-Rafiki zako kushiriki kwa yale yanayokupendeza katika programu katika tovuti za kijamii kama vile face book na twiter na nyinginezo.

  Kama ambavyo ‘Tatbiiq’ hii imefasiriwa kwa zaidi ya lugha tano, nazo ni: (Kiingereza, Kifaransa, Kichina, Ki-indonesia, Kibengali, Kifursi, Kirusi, Kitajiki, Kiurdu, Kihausa, Kiswahili, Kihispania, Kireno, Kijerumani, Kihamhari) baadhi zimeshateremshwa na nyinginezo zinafuatia utekelezaji wake InshaAllah.

  Fiqhi ya Ibada iliyokuwa na picha-Ni lazima kwa Kila nyumba ya Muislamu